CHONGOLO AIPONGEZA HALMASHAURI YA KALAMBO KUANZISHA TEKNOLOJIA MPYA YA UKAUSHAJI WA DAGAA NA SAMAKI
Na Neema Mtuka. Mkuu wa mkoa Songwe Mhe.Daniel Chongoro ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa kwa kuanzisha teknolojia mpya ya UKAUSHAJI wa DAGAA na SAMAKI kwa kutumia kaushio la kisasa (Solar tent drier)ambalo litawezesha upatikanaji wa samaki na dagaa wenye ubora na kuwezesha wavuvi kujikwamua na Hali ya kiuchumi. Ameyasema hao baada ya kutembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya Kalambo kupitia maonesho ya wakulima nanenane yanayofanyika kikanda jijini Mbeya na kuipongeza Halmashauri ya Wilaya Kalambo kwa kuanzisha teknolojia hiyo ambayo itawezesha kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi baada ya kuvuliwa hususani kipindi Cha masika. Awali akitoa taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo Shafi Mpenda ,Afisa uvuvi Wilayani humo Bw.Abdul Balozi,Amesema sambamba na teknolojia hiyo pia wameleta bidhaa mpya ya unga wa samaki ambayo ni ya kwanza kwa Kanda ya nyanda za juu kusini ambayo itasaidia kupunguza udumavu na utapiamlo kwa watoto kutokana na u...