UTPC KUENDELEA KUELIMISHA UMMA,UMUHIMU WA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo amesema ili kusaidia kupunguza hali ya uhasama dhidi ya Waandishi wa Habari UTPC inaendelea kutumia Klabu za Waandishi wa Habari mikoani kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa Uhuru wa vyombo vya Habari na jukumu la Waandishi wa Habari katika jamii. Nsokolo ameyasema hayo Leo Novemba 2,2023 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku ya Kimataifa ya kukomesha Uhalifu dhidi ya Waandishi wa Habari ulioandaliwa na UTPC na kufanyika kwa njia ya mtandao(Zoom). Amesema maadhimisho hayo kwa mwaka 2023 yanalenga Kuongeza uelewa kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo Waandishi katika kutekeleza majukumu Yao,lakin pia kuonya juu ya kukithiri kwa vitendo vya kikatili na ukandamizaji dhidi ya Waandishi wa Habari. Aidha akiongelea kujenga Mazingira salama kwa Waandishi wa Habari amewashukuru ubalozi wa Uswiss hapa Nchini Tanzania,kwa ufadhili wao katika mradi na Mkuu wa jeshi la polisi Nchini IG...