WAZIRI MKUU ATIMIZA AHADI YAKE KWA REYO
Taasisi ya vijana inayojishughulisha na utunzaji wa Mazingira mkoani Rukwa(Rukwa Environmental Youth Organization-REYO)imekabidhiwa Pikipiki ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa mapema mwaka huu alipofanya ziara katika Mkoa wa Rukwa. Amikabidhi Pikipiki hiyo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere ameishukuru ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutimiza ahadi hiyo kwa Taasisi ya REYO. Ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuendelea kutunza Mazingira na kuhamasisha wananchi kutunza Mazingira kwa kutokata miti na kuchoma moto hovyo misitu iliyopo. Akipokea Pikipiki hyo kwa niaba ya Taasisi ya REYO,Be.Issa Rubega amemshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa msaada huo ambao itasaidia kuendelea kampeni Ya utunzaji Mazingira kwa kuwa Pikipiki hiyo itasaidia kufika kwa urahisi na haraka katika maeneo yote.