Mtumishi Halmashauri Ya Kalambo Mbaroni Kwa Kukutwa Na Mashine Bandia Ya Ukusanyaji Mapato.
Na Baraka Lusajo - Kalambo Jeshi la polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Timoth Ngambeki ambae ni mtumishi wa Halmashauri ya Kalambo kwa tuhuma za kutumia mashine bandia na kutoa risiti feki kwa wananchi na kuisababishia serikali hasara ya shilling million thelathini na tisa na laki tano. Mapema akiongea ofisini kwake mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Kalambo Shafi Mpenda alisema mtumishi huyo aligundulika kufanya kitendo hicho baada ya kushindwa kuwasilisha fedha Benk na kwamba baada ya ufuatiliaji zaidi kwenye mageti ya ukusanyaji mapato aligundua uwepo wa udanganyifu kwenye utoaji wa risiti. ‘’baada ya kugundua uwepo wa udanganyifu kwenye swala la ukusanyaji mapato nilianzisha utaratibu wa kuweka madaftari ya kusaini kwenye mageti yote yanayo unganisha halmanshauri za jirani na kuweka watu ambao walikuwa wakifanya kazi ya kupiga picha risiti za ushuru kisha kunitumia na wakati mwingine nilikuwa nikiamka usiku na kufuatilia mwenendo wa ukusanyaji mapato kwenye mag...