MIGOGORO WASABABISHWA KANISA HILI KUFUNGWA
MGOGORO ulioibuka katika Kanisa la Mtakatifu Andrea Kantalamba la Anglikani jimbo la Lake Rukwa lililopo katika Mtaa wa Kantalamba Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa umechukua sura mpya baada ya Serikali kulifunga kwa muda kanisa hilo hadi mgogoro huo utakapotatuliwa. Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba amesema baada ya kukaa na pande mbili zinazosigana katika kanisa hilo amebaini kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu ambao haujapatiwa ufumbuzi na baada ya kuwasiliana na Askofu Mkuu wa Anglikani Tanzania MAIMBO MNDOLWA serikali ya wilaya ya Sumbawanga imeamua kutoa tamko la kulifunga . Waryuba amesisitiza kuwa kanisa hilo halitafunguliwa kwa shughuli yoyote mpaka hapo utakapomalizwa mgogoro huo na askofu Mkuu wa Anglikani na kanisa lolote litakalotokea kuwa na uvunjifu wa amani litafungwa kupisha usuluhishi. Jumapili iliyopita waumini wa Kanisa la Mtakatifu Andrea Kantalamba la Anglikani jimbo la Lake Rukwa lililopo katika Mtaa wa Kantalamba walishindwa kusali katika kanisa ...