RUKWA Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Rukwa Mh.Irene Ndyamkama ameanza ziara yake na kukabidhi mradi wa UWT ambao ni viti 100 vitakavyosaidia kukodisha na kuwaingizia kipato wanachama wa UWT , sambamba na hilo ameahidi kuwalipia Bima ya Afya iliyoboreshwa CHF kwa mwaka mmoja,Ametoa mafunzo ya ujasiliamali na wakufunzi kutoka SIDO kwa lengo la kuwainua wajasiriamali.Mafunzo haya yamehusisha wajumbe mbalimbali kutoka katika kata 9 zilizopo manispaa ya Sumbawanga. Naye msemaji wa Bima iliyoboreshwa CHF Dr. Joseph Ngwale kutoka kiyuo cha Afya Mazwi amezungumzia umuhimu wa Bima hiyo na kuwaasa watu kujitokeza kwa wingi kuweza kupata huduma za afya kwa urahisi pale tu unapohisi afya kuteteleka. Kwa upande wa wanawake waliopata Bima ya afya wameonesha nia ya dhati kuunga jitihada zinazofanywa na mbunge,pia kumpongeza kuwasaidia kupata Bima ya afya iliyoboreshwa.Mbunge wa viti maalumu Mh. Irene Ndyamkama anakutana na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali vya akina mama na kuwau...
Posts
Showing posts from March, 2021