Posts

Showing posts from June, 2020

Wandishi Wa Habari Mkoani Rukwa Wachagua Viongozi Wapya.

Image
KATIKA  PICHA NI WANACHAMA WA RUKWA PRESS WAKIWA KWENYE  CHUMBA CHA UCHAGUZI Na  Baraka Lusajo . Rukwa CHAMA cha Waandishi wa Habari mkoani Rukwa (RKPC) kimepata viongozi wapya watakao kiongoza Chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.  Uchaguzi huo umefanyika Jana kwenye ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga ambapo Waandishi wa Habari walitumia demokrasia yao kupitia uchaguzi ambao uliangaliwa na mjumbe wa bodi UTPC Andrew Kuchonjoma na Mwakilishi wa katibu tawala wa mkoa Emmanuel Kakwezi. KATIKA PICHA NI WANACHAMA WAKIWA KWENYE CHUMBA CHA UCHAGUZI  Mwenyekiti wa Baraza la uchaguzi Cresensia Daimon alimtangaza Swima Ernest kushinda nafasi ya Mwenyekiti kwa kupata kura 17 za ndiyo huku kura 9 za hapana, Makamo mwenyekiti ni Israel Mwaisaka aliyepata kura 13 dhidi ya mpinzani wake Emmanuel Mayunga Aliyepata kura 11,nafasi ya katibu mkuu ilinyakuliwa na Sammy Kisika aliyepata kura 25 za ndiyo ambapo alipata Kura 1 ya hapana kwa kuwa hakua na mpin...